Kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter amesema kuwa  Chelsea hawakuwa na ubora wa kurejea kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United baada ya kupoteza kwa bao 1-0 hapo jana wakiwa ugenini.

 

Potter Alalamikia Uchezaji Duni Kwenye Safu ya Ushambuliaji

Chelsea walifanikiwa kupiga mashuti mawili pekee yaliyolenga lango huku mshangao wa Joe Willock ukiipatia Newcastle pointi 3 muhimu baada ya kupachika bao zuri katika kipindi cha pili cha mchezo.

Potter anakuwa meneja wa kwanza wa Chelsea kupoteza mechi tatu mfululizo za ligi tangu Jose Mourinho alipofanya hivyo mwaka 2015, na kocha huyo wa zamani wa Brighton and Hove Albion alikasirishwa na ushambuliaji wa timu yake.

Potter Alalamikia Uchezaji Duni Kwenye Safu ya Ushambuliaji

Potter huyo aliiambia Sky Sports kuwa; “Kulikuwa na makosa mengi, tulikuwa na ubora wa kucheza lakini tulikosa kiwango cha mwisho. Ncastle wanajiamini sana na tulirejea kipindi cha pili kwa juhudi za Conor lakini wakafunga bao.”

Aliongeza kwa kusema kuwa ulikuwa mchezo mkali, huku na tupo katika wakati mbaya na msururu huu wa hasra umekuja katika mechi tatu za mwisho za ligi kabla ya Ligi kusimama kwa kombe la Dunia.

Potter Alalamikia Uchezaji Duni Kwenye Safu ya Ushambuliaji

Chelsea imekuwa na kipindi kigumu na kumekuwa na mazuri mengi lakini pia mabaya na wakati mwingine lazima ukubali mapambano uliyonayo. Na hapa ni kuhusu kujipanga upya na kuanza tena, ni nusu ya pili ya msimu na kuna safari ndefu.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa