Mechi ya Watani wa Jadi ambayo Yanga na Simba wanaikumbuka sana ilikuwa ni mechi ambayo Yanga ikishinda au kupata sare inakuwa Bingwa wa ligi, Simba ikipoteza mechi inashuka daraja!

Hiyo ilikuwa mwaka 1988, Simba ilikuwa na alama 20 nafasi ya tatu kutoka mkiani wakiwa kwenye hatihati ya kushuka daraja. Yanga ilikuwa inakimbizana na Costal Union kuwania ubingwa.

simba
Msimamo wa Ligi

Ndipo timu hizi zikakutana kwenye mchezo wa Watani wa Jadi, kumbuka Yanga ikishinda inakuwa bingwa na Simba akipoteza anashuka daraja.

Wananchi walihitaji alama moja pekee kushinda ubingwa kwa sababu Coastal Union ilishapoteza mechi dhidi ya African Sports.

Simba ilitangulia kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Edward Chumila lakini wananchi wakasawazisha kupitia kwa Issa Athumani.

simba

Kipindi cha pili Simba ilipata bao la pili lililofungwa na John Makelele na mechi ikamalizika Mnyama ikishinda 2-1 na kubaki ligi daraja ka kwanza. Yanga ikapoteza ubingwa kwa tofauti ya magoli dhidi ya Coastal Union baada ya kulingana pointi.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

simba, Simba Ilivyonusurika Kushuka Daraja, Meridianbet

SOMA ZAIDI

8 MAONI

  1. Ndipo timu hizi zikakutana kwenye mchezo wa Watani wa Jadi, kumbuka Yanga ikishinda inakuwa bingwa na Simba akipoteza anashuka daraja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa