Fellaini Arudisha Fadhila kwa Timu Yake Ya Zamani

Marouane Fellaini kukopesha klabu yake ya zamani ya Standard Liege ili kutoshushwa ligi daraja la nne. Klabu hiyo ya Ubelgiji tayari ilikuwa kwenye ukata mkubwa wa kifedha hata kabla ya janga la virusi vya Corona ambalo limezidisha hali kuwa mbaya zaidi.

Mnamo mwezi Aprili, Shirikisho la Soka la Ubelgiji lilikataa kuwapa Standard Liege leseni kutokana na klabu hiyo kudaiwa malipo ya mishahara kutoka kwa wachezaji. Klabu hiyo imewaomba wachezaji wake wa zamani kuwasaidia ili kujikwamua katika anguko la kiuchumi walilopo na vyombo vya habari vya Ubelgiji vinaripoti kuwa Fellaini atatoa mkopo wa Euro milioni 2.6 kwa klabu hiyo.

Uwanja wa Timu ya Standard Liege

Nyota huyo wa zamani wa Everton na Manchester United, anaekipiga kwenye klabu ya Shandong Luneng kwasasa ameungana na kiungo wa BVB Axel Witsel kutoa mkopo kwa klabu hiyo. Witsel alicheza Standard Liege takribani michezo 1500 kwa zaidi ya miaka mitano kati ya mwaka 2006-11.

Nyota huyo wa Dortmund kwa kushirikiana na wawekezaji wametoa msaada wa Pauni milioni 1.3 na pia kuchangia asilimia 45 katika maboresho ya uwanja wa klabu, ambayo yamepangwa kufanyika katika miaka ijayo.

Mahakama ya Ubelgiji itatoa uamuzi juu ya hatma ya klabu hiyo tarehe 5 Mei na kwa mujibu wa Bladbe, klabu inahitaji kutafuta nyongeza ya angalau Euro milioni 12 ili kuendelea kuwepo katika ligi kuu kwa msimu ujao.

13 Komentara

    Nimeipenda hii kukumbuka ulikotoka na kusaidia pale penye uhitaji big up big boys

    Jibu

    Nikwel lazma ukumbuke ulipotoka mana ipo cku utakwama utarudi tena.

    Jibu

    Ni vizuri kukumbuka ukipotoka!

    Jibu

    Safii sana ndio inavyotakiwa👍

    Jibu

    Ameonyesha moyo waupendo hongera kwake😘

    Jibu

    Msahau kwao mtumwa big up kwao

    Jibu

    Vizuri kwa kukumbuka ulipotoka

    Jibu

    Ni vizuri

    Jibu

    Nyumbani ni nyumba htaka porini

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Mkataa kwao mtumwa big up💪💪

    Jibu

    Ni wachache sana wanakumbuka walipotoka hongera

    Jibu

    Amefanya Jambo zuri Sana.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.