Lampard akiohojiwa na vyombo vya habari amesema “ Tuna paswa kua moja ya wanaopigania ushindi, tunatakiwa kufanya hivyo kwa namna yetu bila kuiga timu nyingine” Lampard amesisitiza wanatazama zaidi juu ya namna gani wataweza kupunguza tofauti ya point kati yao na timu zinazoshika usukani katika msimamo wa ligi kuu Uingereza kwa njia zao wemyewe walizopanga.

Lampard ameiongoza Chelsea kufikia nafasi ya nne Bora katika msimamo wa ligi kuu kama Kocha mkuu wa timu hiyo licha ya kupigwa adhabu ya kuto kusajiri kwa kipindi cha majira ya joto.
“Sitaki kukimbilia kuwaiga Liverpool na Chelsea kwasababu walicho kifanya kwenye ligi kinajulikana, nitakua mpumbavu sana nikianza kusema naweza kupunguza tofauti ya point kwa kuiga wanavyo cheza, na ieleweke kua kuwaiga ni ngumu kwa maana kumekua na kazi kubwa iliyofanywa na wachezaji na Makocha wa timu hizo mbili.
Lampard ameongezea kwa kusema ataongeza hali ya ushindani na kujiamini kwa wachezaji wake na kuwafanya wawe na nguvu na tayari kwa kupambana.
Kutokana na Janga hili la Korona lililosababisha michezo mingi kufungiwa , Lampard amekili kua kunahitajika sana hali ya kujamini kwa wachezaji wake kwa kujiweka vyema kwa mazoezi na kusisitiza kua wachezji walio umia watarudi wakiwa na nguvu pindi janga hilo litakapo Koma.