Mshambuliaji wa Udinese Stefano Okaka anatarajia kupata nafasi nyingine ya kukipiga timu ya taifa ya Italia. Staa huyu anasema kuwa anacheza soka kwa ajili ya mashabiki na anabainisha kuwa mambo mengi mazuri yapo njiani.
Udinese wameshikilia nafasi ya 14 kwenye ligi ya Serie A ambayo imesimamishwa, walitoa sare katika mechi zao 4 mfululizo wakati ligi ikielekea kusimama. Okaka alikuwa na mchango wake mkubwa hapa.
Okaka aliwafungia goli Italia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Albania Novemba 18, 2014. Ameichezea timu ya taifa ya Italia mara 4 mpaka na mara ya mwisho alicheza mechi ya Italia dhidi ya German march 29, 2016.

Staa huyu anatarajia kuwa anaweza kupata nafasi ya kuonesha uwezo wake zaidi katika kikosi cha taifa hilo, baada ya kufanya vyema msimu huu. Okaka anasema kwa sababu amefunga magoli 11 na kutoa asisti 3, basi amejitahidi kufanya vyema kuliko wachezaji wengi wanaotajwa.
Staa huyu anatamani ligi imalizike, hata kama itakuwa ni bila mashabiki. Anakubali kuwa mechi bila mashabiki haitakuwa kama wakati mwingine lakini ni bora kuliko kutokucheza kabisa.