Nyota wa Real Madrid Eden Hazard ameweka wazi aina ya maisha ambayo anayaishi kwa sasa akiwa karantini. Nyota huyu wa zamani wa Chelsea, ameweka wazi kuwa anakutana na changamoto kwenye kula vyakula kwa ajili ya Afya yake.
Kwaida wachezaji wanatakiwa kuchunga sana aina ya chakula wanachokula ili kuepusha kupata uzito wa haraka utakao athiori ucheezaji wao dimbani. Nyota huyu aliambia RTBF kuwa anajikuta anashindwa kujizuia kula sana, hasa maandazi!
“Inakuwa ngumu sana kwangu, najaribu kutokula sana. Najitahidi nisiende kula sana maandazi, lakini haiwi rahisi.” -Hazard
Suala la Uzito wa Hazard
Suala la kuongezeka uzito linawatia wasiwasi mashabiki wengi wa Real Madrid, maana huathiri kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa mchezaji anapokuwa uwanjani.
Hazard alitajwa kuwa aliongezeka uzito maradufu alipofika Real Madrid. Nyota huyu alibainisha kuwa msimu uliopita aliongezeka zaidi uzito.
“Siwezi kuficha, ninapokuwa likizo, nakuwa likizo. Mimi ni aina ya wale watu ambao wanaweza kuongezeka uzito haraka na pia kupungua haraka. Nilipokuwa na miaka 18 nikiwa na Lille, nilikuwa na uzito wa kilo 72. Msimu huu wa joto nilipanda hadi kilo 80 na nikashuka kwa siku 1o tu” -Hazard
Jeraha lake la enka
kabla ya ligi kusimama, alikuwa na jeraha la enka, na kwa sasa anaendelea na matibabu akiwa nyumbani huku akipata maelekezo ya mtalamu wake kupitia mtandao.


Gabriel
Good news 👍