Hapa Hamna Usiyempenda!

Duniani kuna aina fulani ya wachezaji ikitokea kuna mmoja wapo unamchukia yupo mwingine ambaye kwa namna youote ile lazima umpende. Hii ni kutokana na ushindani, uwezo au kuna wakati aliwahi kuipa timu matokeo na kumwona kama msaada mkubwa sana kwenye timu husika. Baadhi ya wachezaji wanaopendwa kutokana na historia zao na makubwa waliyowahi kuyafanya miongoni mwao ni:

Marco Reus

Ni miongoni mwa wachezaji waaminifu kuwahi kutokea pale Dortmund, amecheza na akina Lewandowski na Matts Hummels ambao baadae walitimkia Bayern Munich. Pia amecheza na Mario Gotze ambaye aliondoma klabuni hapo lakini baadae aliweza kurejea tena. Mwaka 2016 alisaini kandarasi nyingine ya kuitumikia klabu hiyo pamoja na kusumbuliwa mara kadhaa na majeraha yanayomfanya akae nje mara nyingi.

Cristiano Ronaldo

Bila shaka asingekuwepo mchezaji huyu kusingekuwepo na majadiliano ya nani ni bora duniani. Wengi tunabishana na kuibua mijadala ya nani mchezaji bora duniani kwa sababu ya uwepo wa hawa wachezaji. Ni mchezaji mkubwa mwenye rekodi nyingi, uwezo wa kufunga na kuipa morali timu. Pia, pamoja na makubwa hayo hana historia nzuri kwenye kombe la dunia kwa sababu hajabahatika kabisa kulishinda.

Lionel Messi

Uwepo wake ni chachu kubwa kwenye soka kutokana na uwezo wake wa pekee katika kuuchezea mpira na katika utoaji wa pasi. Ni mchezaji ambaye haitaji mjadala sana katika mchango wa mataji ndani ya klabu ya Barcelona kwa kipindi kirefu. Anachokikosa hadi sasa ni kama ilivyo kwa mpinzani wake wa kisoka, Ronaldo naye anakosa kikombe kikubwa cha dunia.

Cesc Fabregas

Ni zao la mzee Wenger hadi leo ana historia kubwa alizoziweka. Ni mchezaji anayejua kuchora pasi za hatari na zenye kumfanya mtu asishughulike kufunga. Amefanya makubwa ambayo hayapimiki kiuhalisia akiwa na Arsenal pia baada ya kutimkia Chelsea aliweza kujenga historia ya ajabu akiwa na klabu hiyo. Ataendelea kuwa historia kwenye soka.

Robin Van Persie

Amefanya makubwa ambayo katika soka hayana upinzani tangia akiwa na Arsenal hata baada ya kutimkia Manchester United; alikuwa anajua goli liko wapi na nini anatakiwa kukifanya akiwa eneo hilo. Jina lake litaendelea kusalia kwenye historia.

2 Komentara

    Wote nawakubali.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe