Ac Milan Waipasua Empoli

Klabu ya Ac Milan imefanikiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa bila katika mchezo wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A uliopigwa mapema leo ugenini katika dimba la Empoli.

Ac Milan ambao waliingia katika mchezo huo wakihitaji ushindi na kuendelea kujiimarisha katika msimamo wa ligi hiyo, Ambapo mpaka sasa wanakamata nafasi ya tatu nyuma ya vilabu vya Inter Milan na Juventus.Ac MilanMabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Italia walionekana kuanza mchezo huo kwa kasi wakihitaji kupata goli mapema, Huku wakifanikiwa kupata goli hilo mapema dakika ya 11 kupitia kwa kiungo Reuben Loftus Cheek.

Mchezo huo uliendelea kua na kasi ambapo vijana wa kocha Stefano Pioli walionekana kuitaka mechi kwelikweli ambapo dakika ya 31 Olivier Giroud aliongeza bao la pili kwa klabu hiyo na kuwafanya Milan kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao mawili.Ac MilanKipindi cha pili kielendelea kama ambavyo kipindi cha kwanza kiliendelea ni Ac Milan kuendelea kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa, Huku wakifanikiwa kupata bao lao la tatu katika mchezo huo dakika ya 88 kupitia kwa Chaka Traore aliyeingia kuchukua nafasi ya Rafael Leao na kuwakikishia Milan alama tatu muhimu.

Acha ujumbe