Infantino Awataka Mashabiki Kuacha Ubaguzi

Rais wa shirikisho la mpira duniani Gianni Infantino amewataka mashabiki wa mpira wa kuacha kufanya vitendo vya ubaguzi wa rangi baada ya Samuel Umtiti na mchezaji mwenzake Lameck Banda kufanyiwa ubaguzi.

Klabu ya Lecce ilifanikiwa kupindua meza katika mchezo wa ligi kuu ya Italia Serie A na kushinda mabao mawili kwa moja dhidi ya Laziomchezo uliopigwa jana, Ndipo mashabiki wa klabu ya Lazio walipowafanyia ubaguzi wachezaji wawili wa Lecce wenye asili ya Afrika akiwemo beki wa zamani wa Barcelona Samuel Umtiti na Lameck Banda.infantinoMechi hiyo ambayo ilisimamishwa kwa dakika kadhaa na mwamuzi wa mchezo huo Livio Marinelli kutokana na mashabiki wa Lazio kuimba maneno yanayoashiria ubaguzi, Huku tangazo likitoka uwanjani kua kama wataendelea kuimba basi mchezo huo hautaendelea.

Rais Infantino hajafurahishwa na kitendo hicho kilichofanywa na mashabiki wa klabu ya Lazio juu ya wachezaji hao wa Lecce, Kitu ambacho kimemfanya kukemea kitendo hicho kwa sauti kubwa na sio kwa mashabiki wa Lazio tu bali mashabiki wote wa mpira.infantinoRais wa klabu ya Lecce ameungana na rais wa Fifa Infantino kukemea kitendo cha kibaguzi ambacho kimefanywa na mashabiki wa Lazio katika mchezo huo, Umtiti pia amepokea ushirikiano kutoka kwa wachezaji wengine wenye asili ya Afrika wakikemea jambo hilo kama Jerome Boateng, Lacazzete, na Naby Sarr.

Acha ujumbe