Inter Milan Yaisambaratisha Ac Milan Derby de la Madonina

Klabu ya Inter Milan imewasabaratisha vibaya wapinzani wao wa jadi Ac Milan katika mchezo wa ligi kuu ya Italia Serie A uliopigwa leo katika dimba la Giuseppe Meazza.

Klabu ya Inter Milan imeweza kuifunga klabu ya Ac Milan kwa mabao matano kwa moja katika mtanange huo mkali uliopigwa jioni hii na kushuhudiwa na melfu ya mashabiki katika jiji la Milan.inter milanVijana wa kocha Simeone Inzaghi wameonekana kuendeleza moto ambao walimaliza nao msimu uliomalizika ambapo walicheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Manchester City na kupoteza kwa bao moja kwa bila.

Katika mchezo wa leo Inter Milan wameonekana kuitawala sana Ac Milan na kufanikiwa kuifunga kwa mabao matano kwa moja wapinzani wao, Huku mabao yao yakifungwa na Henrikh Mikhtaryan aliefunga mawili na mshambuliaji Marcus Thuram,Hakan Calhanoglu pamoja na Davide Frattesi bao la kufutia machozi la Ac Milan likifungwa na Rafael Leao.inter milanKlabu hiyo mshindi wa Copa Italia msimu uliomalizika na washindi wa pili katika ligi ya mabingwa ulaya msimu uliomalizika wamekua na asilimia 100 za ushindi msimu huu kwani wamefanikiwa kushinda katika michezo yao yote minne ya ligi kuu ya Italia waliyocheza mpaka sasa na wanaongoza ligi wakiwa na alama 12.

Acha ujumbe