Klabu ya Juventus inapanga kumpa mkataba wa muda mrefu kiungo wake raia wa kimataifa wa Italia Manuel Locatelli ambaye alikuja klabuni hapo kwa mkopo kwa mara ya kwanza.
Manuel Locatelli amekua kwa mkopo klabuni hapo kuanzia mwaka 2021 akitokea klabu ya Sassuolo ambayo nayo inakipiga nchini Italia katika ligi kuu ya Italia Serie A.Klabu ya Juventus inataka kuendelea kua na mchezaji huyo kikosini na hiyo ni baada ya kuonesha kiwango bora tangu atue klabuni hapo mwaka 2021 na kuwavutia mabingwa hao wa zamani wa Italia.
Manuel Locatelli anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka ndani ya viunga vya Allianz mpaka mwaka 2028, Mkataba huo unatarajiwa kusaini siku ya Alhamisi ndani ya wiki hii.Klabu ya Juventus wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanairejesha klabu hiyo kwenye ubora ambao ilikua nao miaka kadhaa nyuma wakitawala soko la Italia, Na ndio sababu kubwa ya kuwapa mikataba wachezaji wake wadogo klabuni hapo.