Juventus Yamueka Chiesa Sokoni

Klabu ya Juventus imemueka sokoni winga wake matata raia wa kimataifa wa Italia Federico Chiesa kuonesha nia yao ya dhati ya kutaka kumuuza winga huyo.

Federico anamaliza mkataba wake mwezi Juni 2025 na klabu ya Juventus hawana mpango wa kumuongezea mkataba nyota huyo, Huku ikiwa ndio sababu ilifanya wamueka sokoni majira haya ya kiangazi kwakua asipouzika dirisha hili kuna wasiwasi wa kuondoka bure klabuni hapo.juventusFederico Chiesa amekua historia ya kupata majeraha mara kwa mara ndani ya klabu hiyo tangu mwaka 2022, Jambo ambalo limewafanya vibibi vizee vya Turin kuona ni wakati sahihi wa kuachana na winga huyo kwakua amekua akipatikana mara chache sana kiwanjani.

Kiasi cha Euro milioni 25 tu ndio kitaweza kumuondoa Federico Chiesa ndani ya viunga vya Turin kwakua ndio kiasi ambacho klabu ya Juventus imekiweka kwa timu yeyote ambayo itamuhitaji Chiesa, Kiasi ambacho kinaonekana kua kidogo kwani winga huyo ukiweka mbali majeraha yake ni moja ya mawinga bora sana barani ulaya.

Acha ujumbe