Nahodha wa Roma, Lorenzo Pellegrini amerejea mazoezini na wachezaji wengine wa kundi la kwanza siku ya jana, siku mbili tu kabla ya mchezo wa Derby della Capitale uliotarajiwa dhidi ya wapinzani wao Lazio kwenye Uwanja wa Stadio Olimpico.
Kulingana na habari zilizotolewa na Tuttomercatoweb, Pellegrini atafanyiwa vipimo na tathmini leo ili kufafanua iwapo ataweza kucheza siku ya kesho.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Pellegrini hajapatikana kwa Jose Mourinho na Giallorossi kwa zaidi ya mwezi mmoja, baada ya kuchechemea dakika 11 katika mechi yake kipindi cha pili dhidi ya Servette kwenye Ligi ya Europa mnamo Oktoba 5.
Baadaye ilithibitishwa kwamba alikuwa amepata jeraha la misuli, ambalo lilihitaji kurekebishwa badala ya upasuaji wa aina yoyote.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Pellegrini kisha alilazimika kukosa mechi za hivi majuzi za kimataifa za Italia dhidi ya Uingereza na Malta mnamo Oktoba.
Nahodha huyo wa Giallorossi ameweza kushiriki katika mechi tano pekee kati ya 15 za Roma katika mashindano yote hadi sasa msimu huu, nne kati ya hizo zikiwa kwenye Serie A, nyingine ikiwa ni mchezo dhidi ya Servette kwenye Ligi ya Europa.