Napoli Yampa Kocha wa Slovakia Kazi

Klabu ya Napoli kwa mara ya pili msimu huu inaachana na makocha wake na hii ni baada ya kuachana na kocha wake Walter Mazzari na kumpa mkataba kocha wa timu ya taifa ya Slovakia.

Klabu ya Napoli imekua haina muendelezo mzuri tangu kuondoka kwa kocha Luciano Spalletti mwisho wa msimu uliomalizika, Hivo baada ya kuondoka kocha huyo klabu hiyo bado haijafanikiwa kurudi kwneye ubora wake.napoliMabingwa hao watetezi wa Serie A wameamua kuachana na kocha wake Walter Mazzari na hii ni miezi minne baada ya kuachana na kocha Rudi Garcia mwezi wa kumi mwaka jana, Ni wazi hii inaonesha ishara mbaya kwa klabu hiyo ambao ni mabingwa watetezi wa Italia.napoli

Klabu ya Napoli inaelezwa kumpa mkataba kocha Francesco Calzona kutoka timu ya taifa ya Slovakia ambapo atakua ndani ya klabu hiyo mpaka mwisho wa msimu huu,Maamuzi haya yamefanyika kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya klabu ya Barcelona.

 

Acha ujumbe