Mchezaji Yanga Afufukia Polisi

NYOTA wa Yanga, Joseph Guede, baada ya masimango mengi kutoka Kwa mashabiki kuwa hafungi, hatimaye amejibu maswali hayo mbele ya Polisi Tanzania jana usiku dhidi ya Polisi Tanzania ya Championship. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

Guede Yanga

Guede alitumia vema pasi ya Augustine Okrah na kutoa gundu la kutoifungia Yanga licha ya kucheza mechi takribani tatu, ilikuwa ni kwenye mchezo wa Azam Sports Federation uliochezwa Azam Complex Chamazi.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 5-0 Polisi Tanzania, Wananchi wakisonga hatua ya 16 Bora na Polisi wakifungashiwa virago kwenye mashindano hayo. Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Guede alifungua pazia kwenye kutupia ndani ya uzi wa Wana Jangwani alitupia mabao mawili dakika ya 13 na dakika ya 45 kwa pasi za Okra.

Farid Mussa alitupia bao moja dakika ya 33 na nyota Clement Mzize alifunga bao moja dakika ya 82 akiwa ndani ya 18.

 

Farid Yanga

Mzize alisababisha penalti dakika ya 85 ilifungwa na Shekhan Ibrahim ikiwa ni bao lake la kwanza ndani ya Yanga akiweka wazi kuwa ni furaha kwake kufanya hivyo. Jisajili na Meridianbet upate bonasi kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

Acha ujumbe