Liverpool, Bayern Kupigana Vikumbo kwa Alonso

Klabu ya Liverpool na Bayern Munich zimeingia kwenye vita kali ya kumuwania kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen Xabi Alonso ambaye anafanya vizuri kwasasa barani ulaya.

Vilabu vya Liverpool na Bayern Munich vyote kwa pamoja makocha wao wataondoka mwishoni msimu huu, Hivo jina ambalo linaongoza orodha ni kocha Xabi Alonso ambaye amefanikiwa klabu ya Bayern Leverkusen moja ya timu tishio barani ulaya kwasasa.liverpoolXabi Alonso ambaye alipewa timu katikati ya msimu uliomalizika akifanikiwa kucheza nusu fainali ya michuano ya Europa League, Huku msimu huu timu hiyo ndio imeimarika zaidi ambapo mpaka sasa inaongoza ligi kuu ya Ujerumani kwa tofauti ya alama 8 mbele ya klabu ya Bayern Munich.

Mpaka sasa ni klabu moja tu ambayo haifungwa mchezo wowote kwenye michuano yote katika ligi kubwa tano barani ulaya na ikiwa sio klabu nyingine ni klabu ya Bayern Leverkusen chini ya mkufunzi Xabi Alonso.liverpoolKocha huyo ambaye ni gwiji wa vilabu vyote vya Liverpool pamoja na Bayern Munich ana mkataba na klabu ya Bayern Leverkusen, Lakini kuna kipengele kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuondoka kama tahitaji kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Acha ujumbe