Liverpool Yaendelea Kuandamwa na Majeraha

 Klabu ya Liverpool imeendelea kuandamwa na wimbi la majeraha kwa wachezaji wake baada ya kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp kuweka wazi idadi ya wachezaji wenye majeraha klabuni hapo.

Kocha wa Liverpool Klopp akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Luton Town akisema wachezaji kadhaa watakosekana kwa mchezo huo akiwemo Diogo Jota aliyepata majeraha wikiendi iliyomalizika, Allison Becker, Curtis Jones, Dominik Szobozslai, na beki Trent Alexender Arnold.liverpoolMshambuliaji Diogo Jota ambaye alipata majeraha katika mchezo wa wikiendi dhidi ya Brentford atakosekana ndani ya timu hiyo kwa zaidi ya mwezi kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata.

Wachezaji wengine kama Trent, Crtis Jones, Allison Becker, pamoja na Dominik Szobozslai nao watakua nje ya uwanja kwa siku kadhaa, Hili ni pigo kwa klabu ya Liverpool katika kipindi hichi ambacho wako kileleni wanawania ubingwa wa Uingereza.liverpoolKlabu ya Liverpool itakua na mchezo wa fainali ya kombe la Carabao siku ya jumapili dhidi ya klabu ya Chelsea, Hivo kukosekana kwa wachezaji hao ambao karibia wote ni wachezaji wa kikosi cha kwanza ni pigo kwa vijana hao wa kocha Jurgen Klopp.

Acha ujumbe