Klabu ya Liverpool imefanikiwa kufika mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kushinda mchezo wake wa leo dhidi ya klabu ya Brentford.
Liverpool wakiwa katika dimba lao la nyumbani Anfield wameipasua klabu ya Brentford kwa mabao matatu kwa bila na kusogea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.Majogoo wa Anfield sasa wamefanikiwa kufikisha alama 27 wakilingana na Man City na Arsenal ambapo City ana mchezo mmoja mkononi, Lakini Arsenal wao wanazidiwa magoli ya kufunga na kufungwa ndio maana wako nafasi ya tatu.
Vijana wa Jurgen Klopp walionekana kuutaka mchezo kuanzia dakika ya kwanza ambapo walikua wanafanya mashmbulizi langoni kwa Brentford mpaka pale ambapo walipofanikiwa kupata bao lao la kuongoza kupitia kwa Mohamed Salah.Mohamed Salah anaendelea alipoishia kwani leo tena katika mabao matatu ya Liverpool amefanikiwa kufunga mawili na kufikisha mabao 10, Huku akiwa nyuma kwa bao moja kwa kiongozi wa mabao mshambuliaji wa Man City Earling Haaland.