Napoli Wamlilia Kvaratskhelia

Klabu ya Napoli kupitia Rais wa klabu hiyo Ariello De Laurentiis wanapambana kuhakikisha wanambakiza winga wao nyota raia wa kimataifa wa Georgia Khvicha Kvaratskelia angalau mpaka mwaka 2025.

Winga Kvaratskhelia inaelezwa hataki kubaki ndani ya klabu ya Napoli kwa msimu ujao na mipango yake zaidi ni kutafuta klabu nyingine ili aweze kwenda kuitumikia, Lakini Rais wa klabu hiyo mipango yake ni kuendelea kubaki na winga huyo wa kimataifa wa Georgia.napoliMpango mkakati wa klabu ya Napoli chini ya Rais De Laurentiis ni kumuongezea mkataba winga huyo mpaka mwaka 2025 huku pia kumuongezea mshahara ikiwa ni moja kipaumbele, Inaelezwa wanajiandaa baada ya michuano ya Euro 2024 kumalizika ndio watalifanyia kazi suala hilo.

Pamoja na klabu ya Napoli kua bora sana kwenye kuwauza wachezaji wake kwa faida lakini awamu hii mambo yamekua magumu kwao, Kwani wako kwenye hatihati ya kumuachia mchezaji muhimu klabuni kwako kuondoka kwa uhamisho huru kama kiungo huyo hatakubali kusaini mkataba mpya.

Acha ujumbe