Napoli Yaishutumu PSG

Rais wa klabu ya Napoli Aurielo De Laurentiis ameishtumu klabu ya PSG inayoongozwa na Rais Naseer Al-Khelaifi kua imefanya mazungumzo na mchezaji wake kinyume na utaratibu unavyotaka.

Rais De Laurentiis ameishutumu klabu hiyo kufanya mazungumzo na mchezaji wake raia wa kimataifa wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia kinyume na utaratibu ambao unafahamika, Lakini aliendelea kwa kusema sio jambo ambalo limemshangaza katika mpira wa miguu duniani.NapoliKlabu ya PSG imekua ikifanya mazungumzo na winga Khvicha Kvaratskhelia wakimuhitaji akajiunge na klabu yao kuelekea msimu wa 2024/25 jambo ambalo Rais wa klabu ya Napoli ndio amekemea vikali kuhusiana na tabia hiyo ambayo imeonesha mabingwa hao wa Ufaransa.

Napoli bado wana mkataba na mchezaji Khvicha Kvaratskhelia mpaka mwaka 2024 ndani ya viunga vya Diego Armando Maradona, Hivo kuna uwezekano mkubwa tuhuma za Rais wa Napoli zina maana kubwa kwani hairuhusiwi kufanya mazungumzo na mchezaji aliye na mkataba wa zaidi ya mwaka pasipo idhini  ya klabu yake.

 

 

Acha ujumbe