Beki wa klabu ya Bayern Munich na timu ya tiafa ya Ufaransa Benjamin Pavard anatarajiwa kukipiga klabu ya Inter Milan ya nchini Italia ndani ya msimu huu.

Benjamin ianaelezwa hayupo kwenye kikosi cha Bayern leo ambacho kitacheza na klabu ya Augsburg, Kutokana na mchezaji huyo kuweka wazi anataka kutafuta changamoto nyingine nje ya klabu hiyo na Inter wamekubali kulipa kiwango cha pesa.pavardKlabu ya Inter Milan wameelezwa kukubali kiasi cha Euro milioni 32 siku kadhaa nyuma kwajili ya kumpata mchezaji huyo, Hivo ni suala la Bayern kuonesha taa ya kijani ili kumuachia kiungo huyo ajiunge na miamba ya soka nchini Italia.

Beki huyo raia wa kimataifa wa Ufaransa ameonesha wazi haitaji kubakia ndani ya kikosi cha Bavarians,Bayern wenyewe wameonesha kukubaliana na mchezaji kutokana na kukubali kiwango cha pesa kilichotolea na Inter Milan.pavardKikao cha mwisho kinatarajiwa kufanyika jijini Bayern baina ya vilabu hivyo viwili kwajili ya kukamilisha dili hilo, Beki Benjamin Pavard alikua anahusishwa na Manchester United lakini ni Inter Milan ambao wamefanikiwa kufikia kiwango kilichokua kinahitajika.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa