Zaniolo Kutimkia Galatasaray

Kiungo wa klabu ya As Roma inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Nicolo Zaniolo inaelezwa ana mpango wa kutimkia klabu ya Galatasaray ya nchini Utruki baada ya dili lake kuelekea nchini Uingereza kufeli.

Kiungo Nicolo Zaniolo alikaribia kujiunga na klabu ya Bournamouth lakini dili lake kujiunga na klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza lilishindikana siku za mwisho kabla ya dirisha kufungwa, Hivo kwasasa kiungo huyo ana mpango wa kutimkia kwa miamba ya soka nchini Uturuki klabu ya Galatasaray.zanioloKlabu ya As Roma na Galatasaray wapo kwenye mazungumzo ya kuhakikisha dili hilo linakamilika na kiungo Nicolo Zaniolo anaondoka ndani ya klabu ya Roma na kuelekea nchini Uturuki, Mchezaji ameshakubaliana na ofa kilichobaki ni vilabu viwili kukubaliana.

Klabu ya As Roma chini ya kocha Jose Mourinho inaelezwa wako tayari kumuachia kiungo huyo aondoke ndani ya klabu hiyo kwakua alishaonesha kuhitaji kuondoka kwenye timu hiyo, Kiungo huyo alikua moja ya wachezaji muhimu ndani ya Roma.zanioloKiungo Zaniolo anataka kuondoka ndani ya As Roma kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo, Kwani baada ya kiungo huyo kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo mashabiki hawakufurahishwa na kitendo hicho na kuanza kumpa vitisho.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.