Tottenham wameshuhudia matumaini yao ya kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza yakiyoyoma baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Burnley na Chelsea kabla hawajalazimisha sare na Arsenal. Harry Kane anakubali kuwa wamefeli.
Nafasi yao kutwaa taji hili imekuwa finyu zaidi wakiwa nyuma kwa pointi 10 dhidi ya Manchester City ambao ndiyo vinara wa ligi hii kwa sasa. Kane anasema kuwa kiukweli wameshindwa kuinuka katika kipindi muhimu zadid kwa klabu hiyo kwenda sambamba na moto wa ligi hii.
Spurs wanajiandaa kuwa wenyeji wa Dortmund kesho Jumanne wakikutana kwenye gemu ya pili ya mzunguko wa timu 16 wakiwa na ushindi wa bao 3-0 wa gemu iliyopita.
Kane ambaye amechapa magoli 22 kwa msimu huu anasema klabu hiyo inahitaji kuongeza nguvu na kufikia mzunguko wa timu 8 wa Ligi ya Mabingwa utadhihirisha kuwa wamepiga hatua kubwa. Anaamini ushindi dhidi ya Dortmund utadhihirisha kuwa klabu hii inakuwa na kuwa klabu kubwa duniani.

