Wakati Besiktas wakiwa wanamuhitaji golia Loris Karius, boss wa Liverpool yuko tayari kumuacha golia huyo aondoke katika timu hiyo. Wakali hawa Besiktas kutoka uturuki wako katika mazungumzo ya kumnasa golia huyo wakati Liverpool wakiwa tayari kupokea ofa ya mchezaji huyo ambaye mwisho wake bado haujafahamika.
mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa anatarajia ofa ya kuhamia Besiktas. Pia besiktas wakionekana kuhitaji dili ya mkopo kwa golia huyo anayetajwa kupata mrithi wake Alisson Becker aliyekuwa AC Roma kwa ada ya Euro milioni 75.
Mwanzo ilisemekana kuwa liverpool wako tayari kumuacha mmoja kati kati ya Simon Mignole na Loris Karius kuondoka lakini meneja wa liverpool Jurgen Klopp amenukuliwa akisema anafurahi kumuacha golia Loris Karius kuondoka Liverpool.


Povel
Gud news