Taarifa zinadai kuwa United wanajiandaa kufanya uhamisho mkubwa wa paundi milioni 120 kwa ajili ya Paulo Dyabala kama wakimpungia mkono wa kwaheri Lomelo Lukaku klabuni hapo.
Manchester United wanaripotiwa kuwa wanataka kufanya dili la kubadilishana wachezaji na klabu ya Juventus kama Lukaku atasepa kiangazi hiki.
Staa huyu wa Juventus amekuwa akiwavutia Mshetani Wekundu kwa kipindi cha misimu kadhaa na amekuwa akifuatiliwa na klabu hiyo kuziba pengo la Romelo Lukaku ambaye hatma yake klabuni hapo inaonekana kama bado haieleweki.
Moja ya vitu ambavyo klabu hii ilihitaji kujiridhisha katika hatua za kufikiria kumleta nyotsa huyu kutoka Juventus ni pamoja na kujua dau halisi ambalo watalilipa kwa staa huyu.
Hata hivyo Juvemtus wanadaiwa kuwa bado wanaonekana kama hawapo tayari kumpoteza staa huyu na kama watamuuza basi dau linalotajwa ni paundi milioni 120.
Juventus nao wameonesha kuvutiwa na Lukaku na kutajwa kuwa tayari wameshafikiria kumleta staa huyo pale Italia, Lukaku anadaiwa kuwa ni mchezaji anayemkubali sana Cristiano Ronaldo na anatamani kucheza naye kabla staa huyu hajastaafu soka.
Huenda dili la sepa lukaku karibu Dyabala likakamilika na Lukaku akatimiza ndoto yake ya mda mrefu baada tu ya kupunga mkono wa kwaheri United.


Povel tz
Dyabala anakitu atatuoshenya kitu united