Nani Kulipa Kisasi?

 

Siku ya kisasi! Kama ilivyo kawaida Man United wanaenda kukutana na PSG katika mchezo utakaokuwa wa kukata kwa shoka. Huku United akijua fika kwamba yupo nyuma kwa magoli mawili ambayo alifungwa nyumbani kwake na PSG. Hivyo, atatakiwa ama kuyalipa na kuongeza mengine ili aweze kupata nafasi ya kusonga mbele.

Kushindwa kwake kupata ushindi katika mechi hiyo kwa angalau goli tatu bila kuruhusu kwake na hiki ni kitu ambacho kiuhalisia ni kazi sana. United wana kibarua kikubwa kuusaka huo ushindi ili kuaminisha dunia kwamba kuna kitu cha pekee.

Katika mechi iliyopita PSG walikosa wachezaji wao tegemezi ambao ni Cavanni na Neymar Jr. Kati ya hao wawili kuna mmoja uwezekano wake wa kucheza mechi hiyo umepotea kabisa baada ya kupewa muda mwingine wa kuendelea kusalia nje ya uwanja ili kuweza kurejea kwenye uimara wake.

PSG wanarudi uwanjani wakiwa wanawakosa wachezaji wao wengine kama ilivyokuwa katika mechi yao ya awali na kusalia na kikosi kilekile ambacho awali kiliweza kupata ushindi mbele ya mashabiki wa United huku kijana anayewatoa machozi wengi, Mbappe kuutawala mchezo uliopita kwa kasi ya ajabu mbele ya walinzi wa United.

Lakini upande wa pili wa wageni wa mechi hiyo wanakutana na kizingiti kikubwa ndani ya mechi hiyo huku wakitegemea zaidi uchezaji wa mpinzani wake kutokana na kuwakosa nyota wao wengi ambao watakuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa ni majeruhi, baadhi yao ni Sanchez, Herrera, Martial, Lingard, Mata, Darmian, Matic na Jones.

Pamoja na majeruhi hao pia safu ya kiungo inategemewa kucheza bila kiungo tegemezi ambaye yupo ndani ya adhabu ya kutumikia kadi nyekundu aliyoipokea katika mchezo wa awali mara baada ya kufanya kitendo kisicho cha kiuungwana kwa mchezaji mwenzake jambo ambalo bado linahatarisha safari ya United.

Kama hali itaendelea hivi bila mabadiliko ya majeruhi hao wa United kuna walakini kwamba kutakuwa na idadi kubwa sana ya magoli ndani ya mechi hiyo kutokana na aina ya wachezaji watakaokuwa wakizuia safu ya kiungo ya PSG mbayo inaongozwa na mtu mwenye uzoefu mkubwa kama Veratti na ulinzi wa mtu kama Thiago Silva. Kwa hali ilivyo United wana zaidi ya kibarua kuweza kushinda mechi hiyo.

Lakini pia kutakuwa na mechi nyingine ambayo Porto atakuwa mwenyeji wa Roma katika mechi ya marejeano. Ikumbukwe mechi ya awali baina ya wawili hao iliisha kwa Roma kuondoka na ushindi wa magoli 2-1 kitu ambacho bado kinampa nafasi Porto ya kuendelea kujiwekea asilimia fulani za kuweza kusawazisha goli na kuweka mazingira ya kiushindani mbele ya mpinzani wake.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.