Kuna taarifa kuwa meneja wa klabu ya Juventus, Maxi Allegri anatarajia kusepa klabuni hapo kwenye msimu wa joto unaokuja. Klabu ya Juventus wanadaiwa pia wapo kwenye maandalizi ya kumtafuta mrithi
wa nafasi hiyo ikiwa meneja huyu ataondoka klabuni hapo, wanatajwa Guardiola vs Zidane.
Kwa mujibu wa Sport Mediaset kupitia The Sun, Guardiola amekuwa mmoja wa Mameneja waliopo kwenye orodha ya kuchukua nafasi ya meneja huyo ikiwa ataondoka pale Juve.
Allegri ambaye anaripotiwa kuwa mbioni kusepa amekututana na changamoto kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati akiendelea kuwa kinara wa ligi ya Italia, Serie A. Ameshindwa kung’ara kwenye gemu Mzunguko wa kwanza wa Timu 16 na kukubali kichapo cha 2-0 kutoka kwa Real Madrid.
Kusajiliwa kwa Cristiano Ronaldo kwa pesa nyingi toka Real Madrid kuliwafanya watabe hawa wa kule Italia kuwekwa kwenye nafasi kubwa ya kushinda Ligi ya mabingwa Ulaya kama sio kufikia hatua kubwa zaidi.
Sasa wakati meneja huyu akifikiliwa kuwa huenda hali hii itamfanya meneja huyu kuachia ngazi msimu wa kiangazi unaokuja, Guardiola anaonekana kama ndiyo chaguo linaloangaziwa sana kisha Zidane anaingia kwenye hesabu hii pia.
Guardiola alishikilia vyema usukanipale Man City akiwasaidia kuingia kuvunja rekodi ya kutwaa taji La Ligi Kuu Uingereza msimu uliopita. Anatajwa kuwa baada yamda wake klabuni hapo anaweza kuamua kuondoka klabuni hapo na kuungana na klabu nyingine kubwa zaidi.
Hata hivyo, mtu mwingine ambaye anatajwa kuwa kwenye nafasi nya kutwaa madaraka pale Turin ni bwana Zinedine Zidane, staa ambaye alibamba sana enzi zake kama mchezaji. Zidane mpaka sasa yupo huru na hana mkataba na klabu yeyote licha ya kuhusishwa na klabu zingine kadhaa bado yupo kwenye orodha ya Juve.


Furahav
Aende tu.
Povel
Popote kambi