Wazee wa Kupindua Meza…

 

Habari sio zilezile tena, hii Manchester inatukumbusha ile iliyokuwepo miaka ya 2000 chini ya Sir. Alex ambayo haikuwa na wasiwasi kabisa hata ikifungwa magoli matatu ambayo kwao ilikuwa ni suala la kujipanga upya na kurudisha magoli yao yote hadi kuondoka na ushindi tena kwenye mechi husika.

Kile kilichokuwa kinaonekana kama historia kwa sasa kipo kwenye matendo; ambapo sio rahisi kuingia uwanjani kwa sasa halafu utegemee matokeo rahisi mbele ya United inayoongozwa na Ole ambaye anaonekana kukirejesha kwenye hali yake ya awali kikosi hicho ambacho kilionekana kupoteana sana kwa siku za usoni.

Mbali na hilo kikosi hicho kimefanya maajabu katika jiji la Ufaransa kwa kubadili uelekeo wa bendera mara baada ya kufungwa katika mchezo wa awali wakiwa nyumbani na wakati wa marudiano wakafanikiwa kuwapa dozi nzito PSG ambao hawakuamini kabisa kile kilichotokea katika mchezo huo.

Wazee wa Kupindua Meza…

Ilikuwa ni mapema tu mwa mchezo dakika ya pili ya mchezo ambapo Lukaku aliwapeleka mbele na kuanza kuibua matumaini ya United pale alipotumia vyema mpira uliokuwa na vipimo vya aina yake mara baada ya kumzidi mbinu mlinzi wa klabu hiyo, Silva na kufanikiwa kumkwepa mlinda mlango mwenye uzoefu mkubwa kwenye michuano hiyo.

Haikuchukua kitambo ambapo Mbappe aliweza kutumia nafasi aliyopata kwa kutoa pasi iliyoweza kutuniwa vizuri na kufanya ubao wa matangazo kusoma 1-1 katika dakika 30 za mwanzo za mchezo. Jambo ambalo likikuwa bado gumu kwa United kujiwekea nafasi ya kusonga mbele.

Kabla kipindi cha kwanza hakijaisha Rashford alipiga shuti kali ambalo lilionekana ni jepesi kwenye macho ya mlinda mlango lakini mategemeo yakawa tofauti mara baada ya kushindwa kuumudu mpira ule na kujikuta unaangukia katika miguu ya mtu aliyekuwa mbogo kwenye mchezo ule, Lukaku na kujikuta wakiandikiwa goli jingine tena.

Hadi timu zinasogea mapumziko United walikuwa wanaongoza mechi hiyo kwa magoli 2-1 mbele ya maelfu ya mashabiki wa PSG waliokuwa uwanjani hapo kuiunga mkono timu yao hiyo na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-3.

Kipindi cha pili kilikuwa ni chenye kuvutia mara baada mategemeo ya PSG kuonekana yanaenda tofauti kabisa na kile walichokuwa wanakitegemea wao ndani ya mechi hiyo. Huku timu zote zikionekana kushambuliana kwa zamu kutafuta goli la kuwafanya waweze kusonga mbele ndani ya michuano hiyo.

Mambo yakawa tofauti pale Kimpembe alipounawa mpira katika eneo la hatari na kumfanya mwamuzi kutoa maamuzi mazito ya kupigwa penati na kushuhudia Rashford akipiga mpira ulioishia nyavuni baada ya kumshinda Buffon.

 

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Asanteh kwa makala meridianbet!!

    Jibu

Acha ujumbe