Laporta Amkosoa Vikali Xavi Hernandez, Amsifu Hansi Flick

Rais wa FC Barcelona, Joan Laporta, ametoa kauli kali kuhusu kipindi cha Xavi Hernandez kama kocha wa timu hiyo, akidai kuwa gwiji huyo wa zamani alikosa uwezo wa kuirejesha timu katika njia ya ushindi kama anavyofanya mrithi wake, Hansi Flick. Kauli hizo zimekuja baada ya Xavi kutoa shutuma kali kwenye mahojiano aliyofanya akiwalaumu viongozi wa klabu kwa baadhi ya matatizo yaliyotokea wakati wa uongozi wake.

Laporta Amkosoa Vikali Xavi Hernandez, Amsifu Hansi Flick

Mvutano kati ya uongozi wa Barcelona na Xavi umeendelea kuwepo tangu kuondoka kwake klabuni hapo. Hata hivyo, hali ilichukua sura mpya baada ya Xavi kudai kuwa aliahidiwa mambo kadhaa ambayo hayakutekelezwa na uongozi. Laporta alitumia jukwaa la mdahalo wa uchaguzi wa urais wa klabu hiyo kujibu madai hayo na kutetea uamuzi wake wa kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi.

Laporta Amkosoa Vikali Xavi Hernandez, Amsifu Hansi Flick

Laporta alisema alishangazwa na kuumizwa na maneno ya Xavi, lakini alisisitiza kuwa kama rais alikuwa na wajibu wa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya klabu. Kwa mujibu wa Laporta, tofauti kubwa kati ya vipindi vya makocha hao wawili inaonekana wazi uwanjani. Alisema alipokuwa na Xavi aliona timu inaelekea kupoteza, lakini chini ya Flick anaona dalili za ushindi hata kwa kutumia wachezaji wale wale.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Laporta Amkosoa Vikali Xavi Hernandez, Amsifu Hansi Flick

Moja ya hoja kubwa iliyozua mgogoro kati ya pande hizo ni suala la kurejea kwa Lionel Messi mwaka 2023. Xavi alidai kuwa Laporta alizuia dili hilo licha ya kupata kibali cha La Liga, lakini Laporta alieleza kuwa sababu kuu ilikuwa hali ya kifedha pamoja na hofu ya presha kubwa ambayo Messi angekumbana nayo endapo angerudi Camp Nou.

Laporta Amkosoa Vikali Xavi Hernandez, Amsifu Hansi Flick

Aidha, mvutano huo ulihusisha pia masuala ya usajili, ambapo Xavi alionyesha kukerwa na kushindwa kumpata kiungo Martin Zubimendi ambaye sasa anang’ara akiwa na Arsenal FC chini ya kocha Mikel Arteta. Laporta, kwa upande wake, alidai kuwa Xavi alipoteza imani na kikosi alichokuwa nacho na mara kwa mara alilalamikia uwezo wa wachezaji pamoja na maamuzi ya waamuzi, jambo lililochangia uamuzi wa kumfuta kazi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.