Unamkumbuka Lazaro wa Bethania? Binadamu alieishi Karne ya kwanza hapa duniani, anaezungumziwa kwenye Injili ya Yohana? Yule binadamu aliefufuliwa na Nabii Issa bin Mariam baada ya kifo chake ndani ya siku nne?

Anyway wale mashabiki wa kutupwa wa Liverpool wakuitwa Liverpudlian wanadai ile comeback yao dhidi ya Barcelona pale Anfield ni ya pili baada ya maajabu ya ufufuo wa Lazaro.
Kaskazini mashariki mwa England mnamo saa 3:43 usiku, dakika ya 82:50 kwenye dimba la Anfield tayari majogoo wapo mbele kwa bao 4-0 dhidi ya Barca, ni maajabu yaliyo mshangaza kila mtu kuona Liverpool wana sababisha kitu kilichoitwa balaa kwa kipindi hicho.
Wakati uwanja na majukwaa yote ya Liverpool yameamka, kuanzia jukwaa la The Kop, Sir Kenny Dalgish na Anfield Road End kote kumeamka, nyasi za Anfield zinapendezeshwa na Pasi za kuburuza nyasi na kuna muda Liverpool walitengeneza Nafasi, Walikaba na kushambulia bila kuchoka hii ndio Total Football bwana.

Wakati ngoma inaelekea mwishoni wale wahuni wanaomkubali sana Bill Shankly, wakaliamsha goma lao, “The fields of Anfield Road” hii nyimbo ikiwa inaimbwa huwa wanalia, huwa wanachizika, Mwanaliverpool yoyote anaruka huku wakitaja vipenzi vyao, Bill Shankly, Kenny Dalgish ‘King Kenny’ na Paisley
Hii inapopigwa Gerrard anakwambia wale watoto halisi wa Melwood wapo tayari kuweka kichwa mbele ya mguu, ni spirit yao ni kumtaka mchezaji atoe jasho na damu.
Ni saa 4:10 usiku, game imeisha pale Anfield, Liverpudlian wanatoka uwanjani.

