Ligi ya EPL kwa kushirikiana na IFAB imekusudia kuanzisha sheria mpya msimu ujao 2020/21 ambazo zitaathiri utumiaji wa VAR. Bodi ya Chama cha Soka cha Kimataifa (IFAB) imeelekeza mambo mbali mbali kuhusiana na utumiaji wa VAR kwa waamuzi, Mpira wa kushika handball’ na upigaji wa penati.
Sheria ya kwanza inahusu VAR: Uwepo wa VAR – monitors’ uwanjani, kwa maana mwamuzi ataruhusiwa kwenda kuaangalia Marejeo ya tukio kupitia VAR zilizopo uwanjani.
Sheria ya Pili: inahusu handball, Mpira kugusa mkono – kwa bahati mbaya au maksudi: “Endapo Mpira utagusa mkono wa mchezaji anayeshambulia kwa bahati mbaya, basi inapaswa kuadhibiwa tu ikiwa itasababisha goli au nafasi dhahiri kwa mchezaji au timu yake kupata bao,”

“Kwa madhumuni ya kuamua makosa ya mpira wa mikono, ‘mkono’ unasimama chini ya kingo (kwapa).
Sheria ya Tatu: Upigaji Penati – golikipa hatoruhusiwa kutoka kwenye mstari wake kabala ya pigo la penati wala kumtishia mchezaji wakati wa pigo la penati. Pia Kuanzia msimu wa 2020/2021, adhabu ya penati itarudiwa ikiwa tu kipa atatoka kwenye mstari na kuokoa penati.
Hii inamaanisha kwamba ikiwa penati itatoka nje ya lango, haitorudiwa licha ya golikipa kutoka kwenye mstari. Lakini uingiliaji wakati wa kupiga penati utasababisha kurudiwa tena hata kama mpigaji atakuwa amefungwa au kakosa. Sheria za ‘offside’ zinaendelea kubadilishwa kwa sasa kwa lengo la kuondoa kiwango cha makosa kilichojitokeza msimu huu.


Gwiji wa Soka Jack Charlton Afariki Dunia.
[…] Charlton,aliye ichezea timu ya taifa ya Uingereza na kufanikiwa kushinda Kombe la Dunia mwaka 1966, amefariki akiwa na umri wa miaka […]