Mbappe Kwenda Real Madrid ni Suala la Muda tu.

Kiungo wa zamani wa PSG anaamin mshambuliaji wa Ufaransa atatua Santiago Bernabeu hivi karibuni.

Kylian Mbappe atajiunga na Real Madrid “ni suala la muda tu” amesema Jerome Rothen, amekiri kuwa nyota wa PSG angetua Madrid kabla ya mlipuko wa Corona.

Mbappe ataendelea kuhusishwa kutua Madrid, kwani kocha Zidane hajaweka siri kuvutiwa na Mfaransa huyo.

Mbappe ambaye ametokea Monaco na kutua PSG kwa mkopo mwaka 2017, ana mkataba wa hado 2022. Mbappe hawezi kubaki kwa mabingwa hao wa Ligue 1 pamoja na jitihada za kumbakisha.

Mchezaji wa PSG Rothen amesema Mbappe, alikaribia kusaini Madrid kabla ya janga la Corona.

“Nafahamu kutoka vyanzo vinavyotaka kumpeleka Mbappe Real Madrid kila kitu kilikamilishwa, lakini kutokana na kinachoendelea, nafahamu kuwasili kwake Madrid kutahairishwa.”

Rothen ameongeza: “Hakuna namna Mbappe ataongeza mkataba PSG.

“Wameshaweka makubaliano tayari, kwasababu PSG walikubali kumruhusu aende majira ya kiangazi. Kwa mtazamo wangu, ni suala la muda tu.”

4 Komentara

    Angeenda tu.

    Jibu

    Aende tuu

    Jibu

    Kylian kwenda madrid ataua soka lake

    Jibu

    Subiri tuangalie huwamuzi wake mwenyew

    Jibu

Acha ujumbe