Mwanzoni kulikuwa na ripoti kuwa binamu wa mmiliki wa Manchester City Sheik Mansour alikuwa anahitaji kuinunua klabu ya Liverpool na kubainisha kuwa alikuwa kwenye mazungumzo ili aweze kuinunua timu hiyo. Taarifa zilizopatikana hivi karibuni ni kwamba binamu wa mmiliki wa klabu ya Manchester City ameshindwa kuinunua Klabu hiyo kwa thamani ya Euro Bilioni 2. Hata hivyo chanzo cha habari kutoka Liverpool kinadai kuwa klabu hiyo haikuwa ikiuzwa japokuiwa walikuwa wakipokea maombi kadhaa kutoka kwa wanaotaka kununua.
katika kukanusha taarifa kuwa kulikuwa na mazungumzo yeyote yaliyokuwa yakiendelea kwa ajili ya kuiuza timu hiyo chanzo kutoka katika klabu hiyo kimedai kuwa hakuna mazungumzo yanayoendelea isipokuwa kwa masharti sahihi Liverpool itawapokea wawekezaji wachache ambao wanaweza kufanya ubia wa kibiashara wenye manufaa kwa maendeleo timu klabu.


Mariam mtandama
Asante kwa taarifa meridianbet #
Povel
Gud news
Furahav
Habari nzuri