Paolo Guerrero kwa sasa hataweza kuichezea timu yake mpya ya International kutoka Brazili kutokana na hukumu aliyopewa inayoimzuia kucheza soka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Awali mkali huyu alifeli kipimo cha matumizi ya dawa za kulevya hivyo angeshindwa kutinga katika fainali za kombe la dunia kule Urusi. Lakini kwa mujibu wa FIFA mahakama moja ya nchini Uswiswi ilitoa maamuzi ya kisheria yaliyomruhusu Paolo Guerrero kucheza katika fainali za kombe la dunia kule Urusi.
Mahakama kuu ya nchini uswiswi imetoa zuio la Paolo Guerrero kucheza hivyo kuathiri mkali huyu kuichezea timu yake mpya. Paolo Guerrero ambaye ana umri wa miaka 34 sasa mwanzo alipewa adhabu na FIFA ya kipindi cha mwaka mmoja na baadae kupunguziwa kuwa miezi 6. Lakini mahakama ya michezo nchini Uswiswi (CAS) ilitoa hukumu tena ya miezi 14 kutoka miezi 6 iliyotolewa na fifa, mpaka sasa Paolo Guerrero anasubiri maamuzi ya mwisho katika rufaa aliyowasilisha mahakamani kupinga adhabu ya miezi 14 aliyopewa na CAS.

