Klabu ya Manchester United imesema inaunga mkono hoja ya Mamlaka za mpira nchini Uingereza za kujaribu kumaliza msimu wa Ligi Kuu, Kombe la FA na UEFA, katika kipindi hichi cha mlipuko wa virusi vya corona.
“Klabu inaunga mkono kumalizika kwa mashindano ya Ligi Kuu, Kombe la FA na UEFA”, Katika maelezo ya klabu imesema ipo kwenye majadiliano kuhusu mashabiki wenye tiketi za msimu mzima kama mechi zitachezwa bila mashabiki.

Ligi Kuu na EFL ilichukua maamuzi mapema mwenzi Machi kuahirisha shughuli za mpira hadi Aprili 30, na PFA imeandaa mkutano na wajumbe wake ili kuongelea changamoto za kiuchumi zinazozikabili klabu kwasasa.
Katika EFL wao tayari wameweka sera na timu kama Leeds United, ambayo wachezaji na viongozi wamekubali kujitolea kupunguza mishahara yao.
Burnley imethibitisha kuwa itawalipa wafanyakazi wote wa mechi katika kipindi chote cha mlipuko, wakati wachezaji wa Birmingham wameombwa waridhie kukatwa 50% ya mshahara.
Kuhusu tiketi za msimu huu, United wamesema “kama ligi haitachezwa au itachezwa bila mashabiki. Klabu itawapa ofa mashabiki wake katika tiketi za msimu ujao au watarudisha kiasi cha pesa kwa mechi zilizosalia.”
Klabu imethibitisha kuwa hii itakuwa kwa wale waliolipa malipo ya tiketi kabla au VIP kwa mechi kubwa msimu huu”, na iwapo mechi zitachezwa kama kawaida, basi tiketi zitakuwa halali.
“Tunashukuru kwa utulivu wa mashabiki katika kipindi hichi chenye changamoto na tunakaribisha majadiliano na wawakilishi wa mashabiki.
“Tunajua mashabiki hawataki kukosa mchezo wowote utakaochezwa katika miezi ijayo na tutasikitika kama itakuwa hivyo lakini wote lazima tutie juhudi katika kupambana na virusi vya Corona.


Rehema Dickson
Sio mbaya ni uamuzi wake
Zeiyana
Korona imeharibu mambo