Kocha mkuu wa timu ya Arsenal Mikel Arteta, raia wa Uhispania aliyezaliwa katika jiji la San Sebastian mwaka 1983 mwezi Machi. Mikel Arteta (38) aligundulika kua amekumbwa na janga la virusi vya Corona mwanzoni mwa mwezi Machi. Alhamisi ya wiki hii tarehe 26 alizungumza kupitia majadiliano ya moja kwa moja kwa njia ya video na waandishi ameelezea hofu yake juu ya janga la Corona.

Kocha huyo ambae pia aliwahi kuitumikia vilabu mbali mbali Ulaya, kama PSG mwaka 2001 na kuhudumu kwa msimu mmoja kisha kutimkia Rangers alikoshinda mataji mawili ya Premier league na League Cup. Baadaye alipita katika vilabu vya Real Socieadad kabla ya kwenda Everton kwa mkopo mwaka 2005 na baadae kujiunga na Arsenal ambayo sasa anaisimamia kama kocha mkuu.
Katika mahojiano hayo Arteta alisema “mimi niko salama, naweza kusema nimepona kabisa lakini kuna muda nawaza zaidi juu ya wale niliokuwa karibu nao kabla ya kupimwa na kukutwa na tatizo.” -Arteta
Arteta aligundulika kua na virusi vya Corona tarehe 12 mwezi March mara tu baada ya mmiliki wa timu ya Olympiakos, Evangelos Marinakis ambae alijiweka Karibu zaidi na baadhi ya wachezaji wa Arsenal na viongozi wa timu hiyo baada ya mchezo wao wa EUROPA uliochezwa wiki mbili zilizopita.
“Nashauri watu kubaki ndani na kufuata taratibu zilizo wekwa kukabiriana na Corona” -Arteta


Rehema Dickson
Kila jambo ni mpango wa mungu ashukuru yuko hai na afya njema pia
farida ahmadi
Hongera siku ya kuzaliwa