Kocha aliyetua kwa mafanikio na kuirudisha furaha ndani ya kikosi cha Liverpool ndani ya kipindi kifupi tofauti na makocha waliowahi kuwepo kikosini hapo kwa miaka ya hivi karibu, Klopp ametangaza nia yake ya kutaka kustaafu na kuachana kabisa na upande huo wa soka ili angalau aweze kupumzika.
Anaona kabisa kuna haja ya yeye kuwa nje na upande huo wa soka mara baada ya kuhudumu ndani ya soka kwa miaka mingi na mafanikio makubwa yanayoonekana wazi. Mkataba wake na klabu hiyo utamalizika 2022 na baada ya hapo hatazamii kabisa kuongeza kandarasi na klabu hiyo ila anachofikiria ni kujiweka pembeni kabisa.
Kocha huyo siku za usoni alikuwa katika taifa lake kupokea tuzo ya heshima iliyotambua mchango wake mkubwa ndani ya soka mara baada a kunyanyua taji kubwa na lenye heshima sana. Ujerumani wametambua nafasi ya kiongozi huyo wa soka kutokana na mafanikio aliyoyapata kwa kumkabidhi nishani hiyo ya kocha bora kabisa wa mwaka.
Klopp alipoulizwa juu ya miaka yake mitatu anaitazamaje katika soka aliweka wazi kwamba anajiona kabisa kwamba anakwenda kustaafu upande wa soka ili angalau awe huru kwa kipindi hicho na atatumia muda mwingi kutojihusisha kabisa na masuala yanayohusu mpira. Hilo analikazia sana na anaonekana kumaanisha.
Kinachompa heshima kocha huyo mara nyingi ni ile tabia yake ya ndani ya kisalia ndani ya klabu moja kwa kipindi kirefu na kwa mafanikio. Ndani ya Liverpool amepewa kandarasi ya miaka saba, lakini pia ndani ya klabu nyingine kama Dortmund na Mainz alikuwa na mikataba mirefu zaidi ambayo ilichangia sana mafanikio yake.
Maamuzi kama hayo ni sahihi kwa kocha kama Klopp kutokana na mafanikio ambayo hadi sasa anayo, kutokana na sababu kwamba soka ni mchezo wa mawazo sana ndio maana hata msimu wa ligi unapokwisha makocha wengi hushukuru kupungua kwa kashikashi ambazo wamekutana nazo ndani ya ligi.
Hivyo, pamoja na kwamba hajafanikiwa kunyanyua kombe la ligi kuu bado ana kikosi chenye uwezo mkubwa ambacho kinaweza kumwongezea kitu katika maisha yake ya kufundisha soka. Kikubwa ni kusubiri suala la muda pekee kuona kama kweli maamuzi yake yatafanya kazi.


Fatina mfingi
Makala nzur
Issa
Habari njema