Moacir Barbosa Nascmento- Chini ya Mwamvuli wa Chuki ya Wabrazili

Tarehe 16/7/1950 ilianza kama siku nyingine tu , pale mitaani na vijiwe vingi Brazil stori ilikua moja tu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Uruguay pale Estadio de Maracana Rio De Janeiro , inawezekana kocha Flavio Costa alikua kambini na vijana wake akiwapa maelezo mbalimbali kimifumo na kiakili . Katika kikosi cha Wabrazil alikuwepo kipa wao mahiri Moacir Barbosa Nascimento hakika dunia ya chuki ilimfungukia siku hiyo ilichukia kwa miaka 50 mbingu zikamuonea huruma zikamchukua fasta tu ujumbe wake wa mwisho alisema β€œsio kosa langu tulikua 11” , baada ya kufungwa 2-1 na Uruguay kwa wabrazil hii siku kwao ni zaidii ya majanga ya majanga ya Hiroshima , nchi ililia sanaa wananchi walifedheheka hata Pele alikua kijana alilia na kuapa kufanya makubwa…

Dakika ya 79 winga wa Uruguay mwenye asili ya Italia Alcides Ghiggia aliipa timu yake goli la ushidi hapo sasa kina mama , wahuni , warembo na watu wote waliamini kipa wao Nascimento amewachomesha wakamchukia na wakamtenga . Sio watu wazima hata watoto wadogo walilishwa sumu kwamba jamaa aliisaliti nchi nzima Moacir alibeba zigo la lawama haswa kwa niaba ya timu nzima . Ikumbukwe mechi za kwanza brazil iliwapiga Sweeden 7-1 na Spain 6-1 na walihitaji sare tu na kila mtu walijua wanachukua ndoo wakiwa ardhi ya nyumbani iliyobarikiwa utajiri wa soka na ubunifu wa starehe ikumbukwe huko umalaya ni kazi kama kazi zingine . Lawama za kufungwa zilielekezwa kwa watu watatu beki wa kati Bugode beki wa kushoto Juvanal na kipa Nascimento.

Goli alilofungwa Barbosa

Wananchi wa Brazil walikataa kumsamehe jamaa walimuona kama msaliti yaani hata kabuli lake wanalichukia , baada ya Brazil kuchukua kombe la dunia 1970 chini ya Pele jamaa alikua anapita sehemu mama mmoja aliyekua na mtoto wake alimnyooshea kidole na kusema β€œmuangalie mshenzi Yule aliifanya nchi nzima ikalia” . Jamaa anaaminika ni zaidi ya mkosi walijtenga nae kabisa ndugu na jamaa wa karibu walimfariji , pengine kwenye masomo ya mpira hasa kipengele cha imani basi huyu jamaa angelisemwa kama mfano wa mkosi na kipengele cha chuki.

Kupitia kombe hilo la dunia huo mwaka Brazil walitaka kutengeneza dunia yao , kwanza ni kukuza uchumi wao na umaarufu kupitia mpira pili walikua wanazindua uwanja wao mkubwa zaidii ulikua na uwezo wa kubeba mashabiki 200,000 pia kuchukua ubingwa katika ardhi yao mama lakini matarajio yoote yalifutika ndani ya dakika 11 . Mwaka 1962 katika mechi moja alipata maumivu ya misuli alitolewa nje katika uwanja wa Anceto Moscoso wenye uwezo wa kubeba zaidi watu 30,000 lakini ni watu 670 tu walimpa mkono wa kwaheri ilikua mwisho wa mpira wake . Jamii ya Wabrazil ilimuacha jamaa afe bila kulipa deni..

Nascimento alikua ni kitovu cha chuki na mkosi mkosi haswaa , baada ya fainali hizo wananchi wakaingiwa na imani mbaya za kishirikana kwanza ilikua mara ya mwisho kuvaa jezi nyeupe pili ukabila ukaingia sanaa katika timu , walipiga marufuku kipa yoyote mweusi kulinda goli lao hadi mwaka 2006 alipokuja Dida . Tukio la Nascimento kufungwa goli la pili inaaminika ndicho kipindi kibaya zaidii katika historian a mbeba lawama alikua kipa wao , yameandikwa na yamesimuliwa mengi kuhusu hilo tukio kuna muvi inaitwa Anatomy of Defeat iliyoandikwa na Paulo Perdigao alisema β€œndio tukio baya zaidii katika historia ya nchi nzimaβ€œ . Aliajiliwa kama msimamizi wa uwanja wa Maracana alikuta ile miamba aliyoitumia bado ipo na siku walipoitoa walimpa kama zawadi kwa kejeli na alienda kuichoma moto..

Wakati wa maandalizi ya kombela dunia 1994 kocha wa Brazil Mario Zagallo alimkatalia jamaa kuongea na wachezaji aliwapowatembelea kambini iliaminika angeleta mkosi . Tarehe 7/4/2000 Barbosa roho yake ilitenganishwa na mwili na kabla ya hapo alisema β€œBrazil kifungo kikubwa ni miaka 30 lakini nilifungwa kwa miaka 50”. Ya huyu jamaa mengi sanaa.

15 Komentara

    Hahahaha mbona hawajamchukia aliyewafungisha saba mbele ya german machine ila story imenipa kitu ambacho sikuwai kukisikia

    Jibu

    Duuuh kweli muda mwengine inakuwa kama laana sio tu kwake Moacir Barbosa Nascmento kuna muda unaweza kubeba lawama mpaka ukajishangaa, maana usipo timiza wajibu wa watu utajikuta unabeba lawama kama za dunia yote…

    Jibu

    R.i.p inasikitisha sana

    Jibu

    alikuwa fundi sana..tutamkumbuka

    Jibu

    Kocha bora angemuacha barbosa aongee Na wachezaji

    Jibu

    Kocha bora angemuacha barbosa aongee Na wachezaji tu

    Jibu

    Balaa hili ila kocha nae angekua na maamuz magumu tu kwakwel

    Jibu

    Alipata wakati mgumu sana

    Jibu

    Sasa mtu ameshakufa bado walikua wanachukia hata kaburi lake ukatili huo

    Jibu

    Daa inasikitisha Sana walimuwekeachuki sana binadamu atuna roho zakusamehe ila nimpila kufungisha goli sio kusudi ila ndio ivyo bahatimbaya lakini watu awalijui ilo

    Jibu

    Story inanishangaza sanaaa

    Jibu

    Mchezo wa soka Kuna nyakati zinakuwa ngumu na raha yote Ni changamoto

    Jibu

    Kuna muda inabidi wakubaliane na hari harithi

    Jibu

    Jamaa alikufa na deni lake

    Jibu

    Inasikitisha sana ,alipitia wakat mgumu mno.

    Jibu

Acha ujumbe