Serena williams anachukua nafasi ya kwanza kwa wanaspoti wa kike wenye utajiri zaidi. Serena Williams ambaye ni bingwa mara 23 wa Grand Slam anaripotiwa kuwa wa kwanza kwa mastaa wa kike wenyekipato cha juu zaidi akifuatiwa na mastaa wengine ambao ni; Caroline Wozniacki, Sloane Stephens, Garbine Muguruza, Maria Sharapova, Venus Williams, PV Sindhu, Simona Halep, Danica Patrick, Angelique Kerber. Wanaspoti nane kati ya hawa wanacheza tennis.
Hii hapa list ya mastaa hawa matajiri na thamani ya utajiri walionao;
- Serena Williams (tennis) – $18.1m (£14m)
- Caroline Wozniacki (tennis) – $13m (£10.1m)
- Sloane Stephens (tennis) – $11.2m (£8.7m)
- Garbine Muguruza (tennis) – $11m (£8.5m)
- Maria Sharapova (tennis) – $10.5m (£8.1m)
- Venus Williams (tennis) – $10.2m (£7.9m)
- PV Sindhu (badminton) – $8.5m (£6.6m)
- Simona Halep (tennis) – $7.7m (£6m)
- Danica Patrick (mbio za magari) – $7.5m (£5.8m)
- Angelique Kerber (tennis) – $7m (£5.4m)


Issa
Serena lazima aongoze sana kashinda mataji mengi iyo inampa nguvu
Ester jackson
Amastahili hilo
warda
Heee yaani hadi raha nampenda sana Serena hongera kwake