Cristiano Ronaldo alikuwa anafikiria ruhusa kutoka kwa Juan Cuadrado kabla ya kuchukua jezi namba 7 pale juventus. Jezi hii ni jezi ninayoipenda zaidi, anasema Ronaldo ambaye alihamia timu hiyo mwezi uliopita akitokea Real Madrid kwa usajili wa kihistoria katika timu hiyo.
Kwa upande wa Cuadrado yeye alikuwa na furaha tu kwa kumpokea Ronaldo akitokea Real kwenye timu hiyo, Cuadrado ndio alikuwa namba saba, lakini alikiri yeye anafuraha kumkabidhi Ronaldo jezi hiyo. Ronaldo ambaye aliongea na timu, pia akaongea na Cuadrado ili kuinasa jezi namba 7 ambayo anaipenda zaidi. “Ninafuraha sana kwa sababu timu imenisaidia na Cuadrado nae amekubali pia, nashukuru sana Cuardrado” ni maneno ya Ronaldo baada ya kujihakikishia ameibamba jezi hiyo.


Mwajuma
Cr 7 mkali wao
Issa
Ni safi
Povel
Gud news