Manchester United na Barcelona wanavaana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya matokeo ya droo ya robo fainali ya iliyochezeshwa Ijumaa hii, Machi 15. Sio mara ya kwanza kwa miamba hawa kukutana, wanamekutana mara kadhaa kwenye gemu kali katika historia ya soka.
Kwa mara ya kwanza kabisa mabingwa hawa walikutana mwaka 1984 kwenye gemu mbili za Kombe la Washindi wa Vikombe -Cup Winners’ Cup. Ngoja tucheki mechi kadhaa bora kabisa walizokutana wakali hawa.
Man U 3 – 0 Barcelona Machi 1984
Gemu ya kwanza ya mabingwa hawa kukutana uso kwa uso ambayo Man U aliibuka kidedea, Ulikuwa ni usiku bora kabisa kwa Man U wakati wakilipa kisasi cha bao 2-0 walichopokea kwa wapinzani wao kwenye gemu ya kwanza cha waliyocheza kule Camp Nou. Licha ya United kuonekana kama walikuwa wanaenda kupoteza gemu hii, lakini mambo hayakuwa mabo Barca wakiwa na mastaa wao wa wakati ule kama Diego Maradona na Bernd Schuster wakajikuta wameshindwa kufurukuta pale Old Trafford.
Man U 2 -1 Barcelona Mei 15, 1991
Mei 15, 1991 mabingwa hawa walikutana tena kwenye fainali ya Kombe la Washindi wa Vikombe -Cup Winners’ Cup, United walifurukuta kujihakikishia ushindi wa taji ambalo lilikuwa ni taji lao la pili kubwa Ulaya.
Barcelona 4-0 Man U Novemba 2, 1994
Barcelona walijitolea uvivu kwenye Kundi A la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuhakikisha wana wachapa vyema kabisa wapinzani wao; nyota Stoichkov aliwachapia Barca magoli 2, na mbrazili Romario akicheka na nyavu mara moja pia beki wa kati Albert Ferrer akichapa bao la 4 na kuwaacha Man U wakisepa watupu kabisa!
Man U 0-2 Barcelona Mei 27, 2009
Ligi ya Mabingwa Ulaya fainali! Hapa United walikuwa wametoka kumchapa Chelsea kama miezi 12 iliyopita kule Moscow, hapa United walikuwa ni timu ya kwanza kujiwekea mazingira mazuri ya kutetea ubingwa lakini wakakwamishwa na vijana wa Pep Guardiola. Samuel Eto’o ndiye aliyewachapia Barcelona bao la ufunguzi ndani ya dakika 10 tu, na Lionel Messi akacheka tena na nyavu kukamilisha mabao 2-0 yaliyokwamisha ndoto ya Man U kutetea ubingwa. Barca wakafanikiwa kunyakua mataji matatu ya Champions League, LaLiga na Copa del Rey.
Barcelona 3-1 Man U Mei 28, 2011
Hapa messi alipata nafasi ya kuonesha umuhimu wake mkubwa kwa Barcelona ambao waliweza kumshinda mpinzani wao Real Madrid kwenye nusu fainali. Wayne Rooney alijaribu kusawazisha bao lililochapwa na Pedro lakini Messi aliweka mkwaju makini kabisa nyavuni kukamilisha bao 2 kabla David Villa hajamalizia kazi kabisa kukamilisha bao 3-1.
Mtazamo; Man Utd watakuwa wanatafuta zaidi ushindi kwa Lengo la kukataa uteja kwenye gemu za hivi karibuni pia Ole Gunnar atakuwa anatafuta sifa za kuendelea kumuweka karibu na kibarua cha kudumu klabuni hapo baada ya kupoteza matumaini na Ligi Kuu msimu huu.


Povel
Habar njema