Nilivutiwa Nao Kabla ya Kujiunga na Liverpool : Virgil van Dijk

Virgil van Dijk amefunguka kuwa alizingatia mambo mengi kabla ya kuamua kujiunga na Liverpool. Mholanzi huyo pia alikuwa kwenye rada ya Manchester City lakini aliamua kuhamia Anfield mnamo Januari 2018.

Virgil van Dijk

Van Dijk anadai mtindo wa kucheza wa Waajili wake Liverpool ni baadhi ya mambo muhimu katika uamuzi wake. Vijana hao wa Jurgen Klopp walifikia fainali ya Ligi ya Mabingwa ndani ya miezi sita tangu kuondoka kwake kwa Pauni 75m kutoka Southampton.

“Kabla sijafanya uamuzi wa kuchagua Liverpool, niliangalia nyanja zote za vilabu; njia ya kucheza, wachezaji wa timu, hatma pia,” aliiambia BT Sport.

“Jiji, mashabiki, Wachezaji wenza kilikuwa ni sehemu ya kitu kikubwa ya kujiunga na Klabu…Nadhani Liverpool wakati huo nilipofanya uamuzi ilikuwa uamuzi sahihi na ni dhahiri kufikia fainali ya Ligi ya Mabingwa katika miezi sita yangu ya kwanza ilikuwa wazi ni bonasi kubwa na ilinisaidia sana katika ukuaji wangu.”

Virgil van Dijk

Tangu walipofungwa na Real Madrid huko Kiev Liverpool wamejijenga upya na kurejea kwa nguvu na kuwa mabingwa wa Ulaya mnamo Juni mwaka jana… Pia wako mbioni kushinda taji lao la kwanza la Premier league ikiwa msimu utaanza tena.

17 Komentara

    Kwel kabisa Virgil van dijk

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Ni vzr kuwa na mapenzi na timu uichezayo

    Jibu

    Ni bora kawa muwazi na kaonesha mapenzi ya dhati na timu yake.

    Jibu

    Inapendeza kuwa na mapenzi na Tim yako

    Jibu

    iko poa

    Jibu

    One of the Best Defender on world football now.

    Jibu

    Vizur sana

    Jibu

    Beki kisiki.

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Itakua alikua mashabiki wa Liverpool before

    Jibu

    Yap anastail kwl kuwepo pale ni mtu sahh meridian bet tz#

    Jibu

    Best defender kwa sasa

    Jibu

    Vvd 💪

    Jibu

    Iko poa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi sana basi anastahili kuwepo Liverpool maana alikua na mapenzi kabla ata ajaenda kuitumikia Liverpool

    Jibu

Acha ujumbe