Penati ya Man United, UEFA Watoa Neno

Gemu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya PSG dhidi ya Manchester United ilikuwa kali na kuacha matokeo ya kihistoria yaliyokuwa na nafuu kwa Manchester United chini ya Ole Gunnar Solskjaer. Penati ilikuja wakati muafaka kwa United!

Moja ya matukio muhimu ilikuwa ni penati ambayo iliwapa ushindi Man Utd kwenye fakika za majeruhi. Wadau wengi, hasa mashabiki wa PSG walidai kuwa adhabu ile haikuwa sahihi kutolewa kwa wakati ule na kudai kuwa mpira ulifuata mkono. UEFA nao wametoa neno kuhusu maamuzi ya mwamuzi aliyesimamia mechi ya Manchester United na PSG.

Adhabu ya dakika za lala salama iliwaachia maumivu PSG ambao tayari walipiga hatua moja ya kutoboa kwenda gazi inayofuata ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kushinda gemu ya kwanza dhidi ya Man Utd nyumbani kwa bao 2-0, hata hivyo bahati haikulala upande wao wakijikuta wanapoteza gemu hiyo kwa 3-1, nafuu ya ugenini ikiwapitisha United kwenda hatua inayofuata.

UEFA wanakubaliana na maamuzi yaliyofanywa na mwamuzi wa mechi hiyo kwa uasidizi wa VAR na kuwapa Man U penati iliyowazalia tunda jema kwa kuwaacha na tabasamu.

Kwa mujibu wa UEFA mpira ule penati ile ilikuwa halali kulingana na mazingira ya kilichofanyika. Uefa wanamsifia mwamuzi kuwa kwa kuwa hakuweza kuona vizuri aliamua kupata usaidizi wa VAR ili kufanya maamuzi.

 

2 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Nice

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.