Bosi Jurgen Klopp anasema kuwa Liverpool wanapaswa kuwa na mawazo chanya, wanapaswa wafurahie wakiwa wanawafukuzia Manchester City.
Watata hawa baada ya kutoa sare kwenye gemu 4 za Ligi wamejikuta wakiwa nyuma ya Manchester city kwa pointi moja wakiwa na gemu 9 mkononi zilizosalia kwa msimu huu.
Liverpool wanatarajia kuwa wenyeji wa Burnley Jumapili hii wakitambua kuwa kama watapoteza gemu hiyo watakuwa nyuma kwa pointi 4 kama wapinzani wao wakishinda gemu dhidi ya Watford siku ya Jumamosi.
Bosi huyu anasema ka mtazamo wake haoni kama wanahitaji kufanya mabadiliko ya mfumo na mbinu za kuscheza kwa sasa wakati wakiwa kwenye mbio za lala salama za ubingwa wa Ligi Kuu. Wakiwa bado na ndoto inayopumua kiasi chake ya kutwaa taji anasema mabadiliko madogo mno yanaweza kuwasaidia kwenye mpango wao wa kushida gemu zilizopata.
Klopp anasema wanahitaji nguvu ya ziada ili waweze kuwachapa Burnley, wanahitaji kuwa vizuri zaidi. Klopp amesisitiza kuwa wamejiandaa kwa kukubali kuwa wanaenda kucheza gemu ngumu. Liverpool wafurahie jitihada hizo!


Furahav
Huyu kocha yuko vizuri.