Mshambuliaji wa Genoa, Krzysztof Piatek anatarajiwa kuingia AC Milan kuziba pengo lililoachwa na Gonzalo Higuain ambaye tayari anaripotiwa kwenda Chelsea kukamilisha dili lake la mkopo. Piatek anatarajiwa kuwafuata kwa paundi milioni 35.
Piatek mwenye umri wa miaka 23 amechapa magoli 19 katika gemu 21 toka alipojiunga na Genoa kwa ada ya paundi milioni 4 akitokea Cracovia mwezi Julai mwaka jana.
Nyota huyu aliku mchezaji wa pekee, wa kwanza kuchapa magoli 8 nane katika gemu zake sita mfululizo tokea mwaka 1946-50.
AC Milan wanashikila nadasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi ya Italia Serie A, wakiwa nyuma kwa pointi 6 dhidi ya wapinzani wao Inter Milan wanaoshikilia nafasi ya 3. Pia wapo nyuma kwa pointi 22 dhidi ya Juventus.


Issa
Ni moto sana