PSG Wapeleka Ubingwa kwa Wahudumu wa Afya

Paris Saint-Germain wametwaa ubingwa wa Ligi ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1 ambao umemalizika kwasababu ya janga la Corona.

PSG walikuwa pointi 12 juu kwenye msimamo wa Ligue 1 ikiwa michezo 11 imesalia kumaliza baada ya ligi kusimama kama hatua za kuzuia kusambaa kwa Corona.

PSG wamepewa taji la Ligi baada ya Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe kutangaza hakuna matukio ya michezo yatakayoendelea katika nchi hadi Septemba.

Pointi moja kwa mchezo ndio mfumo uliotumika kuamua hatma ya msimamo wa Ligue 1.

Marseille, wakiwa nafasi ya pili, wamefuzu moja kwa moja kwenda Champions League wakati nafasi ya tatu Rennes ataenda kwenye hatua ya mtoanow.

Toulouse na Amiens wameshuhswa daraja kutoka ligi kuu. Lorient wametwaa ubingwa wa Ligue 2 na Lens watapanda daraja kwenda ligi kuu.

Klabu imesema “Tunapeleka kombe hili kwa watumishi wa afya na siku zote hao ndio mashujaa wakiwa mstari wa mbele”.

Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa PSG, Nasser Al-Khelaifi ameongeza kusema watumishi wa afya wamejitoa kwa wiki nyingi wanahitaji kuangalia kwa tofauti”.

Ameendelea: “Tunaelea na kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na serikali ya Ufaransa kumaliza ligi. Kama serikali ilivyosema afya ni kipaumbele cha kila mtu.

“Katika waka ti mgumu, natumaini hili taji litaleta furaha kidogo kwa mashabiki wetu wote. Ni washukuru wote kwa maamuzi yenu kwano mmeisaidia PSG kuendelea kusonga.”

21 Komentara

    Mcheza vizur hutuzwa

    Jibu

    Wamestahili hili taji

    Jibu

    Ila sio maamuz sahih wangecheza ata bila mashabiki ili tuone uhondo

    Jibu

    Wahudumu wa afya wana mchango mkubwa sana hasa kipindi hiki cha Corona.hongera PSG kwa ushindi

    Jibu

    Yaani ubingwa bila kusherehekea daah ili janga cjui litaisha lini mungu atulinde

    Jibu

    Maamuzi yao no bomba

    Jibu

    Hongera zao kwa ushindi PSG

    Jibu

    Wanastahili kabisaaa hao watumishi wa afya nimeipenda hiyo….

    Jibu

    Ni jambo la msingi sana PSG wamefanya ni jambo la kuigwa na wengine pia.

    Jibu

    Amestahili kuchukua ubingwa

    Jibu

    Bora walivyomaliza bwana mana Kurudi kucheza ni ngumu

    Jibu

    Hayo ndo maamuz yalobaki baada ya ufaransa kusimamisha ligi kwasababu ya corona hongera kwa taji PSG

    Jibu

    Kwa kweli afya ni kipaumbelee cha kila mtu

    Jibu

    Na nchi nyingine wanatakiwa wafanye hivyo itakuwa vzur

    Jibu

    Hongera psg kwa ushindi mko vizuri

    Jibu

    PSG walistahili kuchukuwa ubingwa

    Jibu

    Hayo ndo maamuzi mazuri coz Corona nijanga la dunia zima

    Jibu

    Kongole PSG

    Jibu

    Wamestail kwn ligi wametawala wao

    Jibu

    Hongera psg kwa ushindi

    Jibu

    Hongera PSG

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.