Je Ronaldo Atarekebisha Makosa kwenye Fainali ya Coppa Italia

Kwa Cristiano Ronaldo, hakuna kitu kilionekana kwenda sawa kwenye mechi ya nusu fainali ya Coppa Italia dhidi ya AC Milan Jumamosi ya wiki iliyopita. Akikosa penati, mfululizo wa nafasi nyingi akipoteza na kiwango duni kwenye mchezo wa Nusu Fainali, kwa ujumla hakuwa kwenye ubora wake kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Italia dhidi ya AC Milan.

Ronaldo

Ila kwa bahati nzuri nyota huyo mwenye Ballon d’Or 5, game ilimalizika kwa sare tasa (0-0) na Juventus akapata nafasi ya kutinga kwenye fainali ya Jumatano hii dhidi ya Napoli. Ronaldo sasa ana kila sababu ya kuingia katika Fainali ya kesho kupambana kutafuta taji lake la 30 kwa klabu na timu ya taifa.

Kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengi waliocheza nusu fainali ya Coppa Italia, Ronaldo pia alionyesha dalili za kutokuwa fit baada ya kuwa nje ya dimba kwa zaidi ya miezi mitatu wakati wa janga la Corona. Nafasi yake ya kwanza kwenye Nusu Fainali ilianza kwa kukosa penati katika kipindi cha kwanza, ikiwa ni mara yake ya kwanza kukosa tangu Januari 2019.

Ronaldo pia alionekana kupata changamoto ya kujiweka katika maeneo sahihi kutoka kwenye nafasi yake ya kawaida kwenye winga ya kushoto kwenda katikati wakati wa kushambulia. Huku kukiwa na uwezekano wa Gonzalo Higuain kuendelea kukosekana kwenye mchezo wa fainali huko Roma, Ronaldo anatarajiwa kusimamishwa mbele wakati Juventus itakapo kuwa ikitafuta taji lake la 14 la Kikombe cha Italia.

Ronaldo

Juventus inalenga kubeba taji lake la kwanza kati ya matatu inayowinda msimu huu (Trebble), wanashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Serie A, alama moja mbele ya Lazio na pia wanaangalia kupindua matokeo ya bao 1-0 dhidi ya Lyon katika mchezo wa pili wa raundi ya 16 kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kwa upande wa Napoli bado pia wapo kwenye Ligi ya Mabingwa, na Jumatano hii watakuwa wanatafuta kushinda Kombe lao la sita la Italia. Mshambuliaji Dries Mertens katika Nusu fainali aliweka kambani na kuandika rekodi ya mabao mengi katika historia ya klabu ya Napoli..Kesho ataendeleza kuweka rekodi??

38 Komentara

    Safii itapendeza kwasababu Ronaldo anajua nn anafanya

    Jibu

    Cr7 mchezaj mkubwa sitegemeh Kama hatafany makosa Tena Kama yale thnks meridian bet kwa update za michezo na burudani

    Jibu

    Iko vizuri

    Jibu

    Ajitahid kwa kweli

    Jibu

    Huyu jamaa no hatari sana anapoliona kombe uwanjani lazima alibebe

    Jibu

    Kukosa penati sio kwa Ronaldo tu mchezaji yeyote anaweza kosa penati ninaimani ataparform vizuri

    Jibu

    Jambo lilomkuta kwny mech ya ac millan n bahat mbaya

    Jibu

    Cr7 kwa kosa alilolifanya naamini kuwa anaweza kufanya mabadiliko katika timu na hiyo ndiyo storia yake ya kuto shindwa kirahisi

    Jibu

    Aongeze juhudi

    Jibu

    Ronaldo anajielewa sana kwanza heshima kwake

    Jibu

    Aongeze bidiii

    Jibu

    Ronaldo ni mahili katika mpira ila anajisikia sana

    Jibu

    Cr7 mnyama akuna asiye mjua ila bado uwez upo maana si mtu wa kumbeza maana bado ana uwezo mkubwa wa kufanya makubwa zaid

    Jibu

    Cristian Ronaldo ni mchezaji mzuri anajituma mno na anajua nini afanye hawapo uwanjani kilichotokea kwnye mechi ya nusu fainali ni bahati mbaya tyuu kukosa penati

    Jibu

    Kujikwaa sio kuanguaka naamini atafanya vizuri kwani ukiongelea wachezaji bora lazima umtaje huyu mnyama CR7 amefanya maajabu mengi makubwa kwenye huu limwengu wa soka tusubirie tuone atakavyopiga tiktaka

    Jibu

    Ronaldo ni mxhezaji ninayemkibali sana #meridianbettz

    Jibu

    Ronaldo ni mxhezaji ninayemkunali sana#meridianbettz

    Jibu

    Ronald anajitambua Sana namkubali

    Jibu

    Namwaminia CR7 atafanya maajabu#Meridianbettz

    Jibu

    Mchezaji mahiri

    Jibu

    Inawezekana tu

    Jibu

    Ronaldo anaweza

    Jibu

    Ronaldo ni mchezaji mzuri atafanya timu yake iibuke na ushindi kwenye fainal inawezekana

    Jibu

    Ronaldo mtu mbaya

    Jibu

    Ronaldo mbona Leo yupo vizuri jmn.

    Jibu

    CR7 namkubali sana hawez rudia kosa

    Jibu

    Uwenda umri ukamtupa mkono

    Jibu

    Cr7 hupo poa sana

    Jibu

    Ronaldo yupo vizuri naamini atafanikiwa tu

    Jibu

    CR7 mnyama leo anarekebisha makosa yake#meridianabettz

    Jibu

    Ukimuangalia CR7 ni mchezaji anaayeweza kucheka na nyavu kwa wastani wa kila mechi

    Jibu

    Ronald ni mchezaji mahili Sana wa mpira

    Jibu

    Mechi ya kwanza baada ya miezi 3 nje wachezaji bado hawajafanya mazoezi ya kutosha. Hope CR7 atafanya vizuri mechi ijayo#meridianbettz

    Jibu

    Maoni:Cr7 anajitambu,yuko vzuri

    Jibu

    Anajua CR7

    Jibu

    Cr 7 naamini harudiagi makosa atafanya vizuri

    Jibu

    CR7 atafanya maajabu#Meridianbettz

    Jibu

    Cr7yupo vizuri

    Jibu

Acha ujumbe