Ancelotti Agoma Kuzungumzia Mustakabali wake Madrid

Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amegoma kuzungumzia mustakabali wake juu ya kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kuelekea msimu ujao.

Mkataba wa kocha Carlo Ancelotti unamalizika mwishoni mwa msimu huu huku kukiwa na tetesi nyingi kuhusu kocha huyo, Lakini yeye mwenye hajataka kuweka wazi juu ya wapi ataelekea msimu ujao.ancelottiKocha huyo ameulizwa na mwandishi wa habari katika mkutano kuelekea mchezo wao wa ligi ya mabingwa ulaya juu ya mustakabali wake klabuni hapo na kocha huyo amesema “Kuhusu mimi kusalia hapa? siwezi kuzungumzia hilo nakupa nafasi ya kuuliza swali lingine”

Kumekua na minong’ono mingi juu ya kocha huyo kuondoka klabuni hapo na kujiunga na timu ya taifa ya Brazil, Japo mpaka sasa haijathibitishwa upande wowote kwani kocha huyo amegoma kuzungumzia suala hilo na shirikisho la soka Brazil pia halijaweka wazi.ancelottiWiki hii pia kumekua na tetesi kua huenda kocha Carlo Ancelotti akasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika mwezi Juni mwakani, Japo bado haijawa taarifa rasmi kutoka kwenye klabu ya Real Madrid.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.