Beki kinda wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Alejandro Balde amesaini mkataba mpya wa muda mrefu ndani ya klabu hiyo ambao utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2028.
Balde ambaye ameanza kupata nafasi chini ya kocha Xavi amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia jezi ya Barcelona na ataendelea kuonekana zaidi katika dimba la Spotify Camp Nou.
Beki huyo ambaye amepandishwa kwenye timu hiyo akitokea akademi ya klabu hiyo maarufu kama La Masia kutokana na ubora aliouonesha akiwa na timu ya vijana ya klabu hiyo.
Beki Balde kwasasa ndio beki tegemezi wa klabu ya Barcelona upande wa kushoto licha ya umri wake kua mdogo, Kwani beki huyo kwasasa ndio chaguo la kwanza ambapo aliekua beki wa kushoto wa klabu hiyo Jordi Alba ametimkia Marekani klabu ya Inter Miami.
Klabu ya Barcelona ipo kwenye utaratibu wa kuhakikisha wanatengeneza timu hiyo kupitia vijana wadogo na kuirudisha kwenye utawala kama zamani na ndio sababu ya kuwaongezea mikataba vijana wenye umri mdogo ndani ya timu hiyo.

