Perisic Nje Miezi Sita

Winga wa klabu ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Croatia Ivan Perisic anaweza kukosekana nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano mpaka sita kutokana na jeraha la goti.

Majeraha ya goti muda mwingi inafahamika yanachukua muda mrefu na ndio sababu winga huyo anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda unaokadririwa kuanzia miezi mitano mpaka mwisho.perisicWinga huyo atafanyiwa upasuaji kutokana na majeraha yake ya goti ambayo ameyapata na ndio yatamuekea nje ya uwanja kwa kipindi ambapo ataacha pengo kwa klabu yake ya Tottenham Hotspurs na timu ya taifa ya Croatia.

Winga huyo anatarajia kurejea mwezi Machi au Aprili na kuweza kupambana kwajili ya klabu yake, Lakini vilevile kuisaidia timu yake ya taifa ya Croatia katika michuano ya mataifa ya ulaya yatakayopigwa mwakani nchini Ujerumani.perisicMbali na Ivan Perisic siku za hivi karibuni wachezaji wengi sana wamepata majeraha ya goti ambayo yanawaweka nje ya uwanja kwa muda mrefu wachezaji kama Jurrien Timber, Eder Militao, na Reece James wa klabu ya Chelsea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.